DOWNLOAD NITABIBU WA KARIBU BY JOSE WA MAPENDO - MP3, MP4 & LYRICS

Title Nitabibu wa Karibu
Artists Jose Wa Mapendo
Genres Gospel
Country Kenya

Nitabibu wa Karibu Lyrics

Ni tabibu wa karibu tabibu wa ajabu;
na rehema za daima ni dawa yake njema.

Imbeni, malaika sifa za Yesu Bwana
pweke limetukuka jina lake Yesu

Hatufai kuwa hai wala hatutumai
ila yeye kweli ndiye atupumzishaye

Imbeni malaika sifa za Yesu Bwana
pweke limetukuka jina lake Yesu

Dhambi pia na hatia ametuchukulia
Twenendeni na amani hata kwake mbinguni

Huliona tamu jina, la Yesu kristo Bwana
yuna sifa mwenye kufa asishindwe na kufa

Kila mume asimame, sifa zake zivume
Wanawake na washike kusifu jina lake.

Na vijana wote tena, wampendao sana,
waje kwake wawe wake kwa utumishi wake.