DOWNLOAD HUJANIKOMOA BY KUSAH - MP3, MP4 & LYRICS

Title Hujanikomoa
Artists Kusah
Genres Bongo Flava
Country Tanzania

Hujanikomoa Lyrics

Nafsi inasema subiri
Moyo unakataa nenda
Nimeziona dalili
Ipo siku nitadema

Maana kila yakidhiri
Yana jirudia tena
Mi mwenzio na dalili
Mimi siwezi kupona

Labda alinionaga mimi tahira
Sina mbele na sinaga dira
Akashindwa rudisha majira
Kasahau na zile fadhila

Labda si wewe 
Tulokula wote, mpaka tukasazaga
Labda si wewe 
Tulokuwa tukipendana na kuchezaga

Roza dunia mapito wowo
Nakuleza haya yatapita woo
Roza dunia mapito wowo
Nakuleza haya yatapita woo

Haya, mwenzako mimi hujanikomoa
Haya, ni kama akili umeifungua 
Haya, mwenzako mimi hujanikomoa
Ndo kwanza akili umeifungua mama

Kama penzi lingekuwa nguo
Ningelivua nikalitupa mbali mawe
Maana nimekosa hadi chaguo
Nimefanya mema ninapigwa mawe

Maajabu ya Musa
Fimbo kawa nyoka eti ananitisha
Na alisha nisusa
Nami nashukuru bora amenishusha

Ilipofika inabidi
Nizoee baridi wowoo
Leo nalitua penzi

Roza dunia mapito wowo
Nakuleza haya yatapita woo
Roza dunia mapito wowo
Nakuleza haya yatapita woo

Haya, mwenzako mimi hujanikomoa
Haya, ni kama akili umeifungua 
Haya, mwenzako mimi hujanikomoa
Ndo kwanza akili umeifungua mama