DOWNLOAD BOYFRIEND WA DAR ES SALAAM BY LADY JAYDEE - MP3, MP4 & LYRICS

Title Boyfriend wa Dar es Salaam
Artists Lady Jaydee
Genres Afrobeats Afropop
Country Tanzania

Boyfriend wa Dar es Salaam Lyrics

Ooooh sweet music ..

Sio wangu mimi
Bali wa dar es salaama (dar es salaama)
Kila binti mjini
Yeye anapita nae (naaaee)
Yani kila kona kama atembea uchi
Nilidhani wangu
Kumbe wa dar es salaama nzima

Nawaambia kwani
Nmekutana nae eeeh !
Kwa ahadi nyingi muda nikamuazima
Anapenda wengi uyo penzi langu kalizima
Si wakumlilia et anatia aibu uyoooo jamani
Tena kuna na mshkaji wangu wa mbezi
Alimkuta na shangazi  
Wanajidunga Johnny Walker na beer

[CHORUS]
Sio wangu mimi
Bali wa dar es salaama
Kila binti mjini
Yeye anapita nae
Yani kila kona kama atembea uchi
Nilidhani wangu
Kumbe wa dar es salaama nzima

Bibie suma atoke
Sijui nani apande
Huyu nae aende ,ili mwingine aje
Namkumbuka ananda aliokoka
Changanyikiwa akawa kama mateka uuuuhhh
Baby wa dar es salama ooh oo !

[CHORUS]
Sio wangu mimi
Bali wa dar es salaama
Kila binti mjini
Yeye anapita nae
Yani kila kona kama atembea uchi
Nilidhani wangu
Kumbe wa dar es salaama nzima

Hata yule shani alikutana nae
Pete kamvisha na kumdunga mimba (euuh euuh)
Muda si mrefu yu karibu kujifungua
Kapata habari bwana yule anaoa kwingine
Namkumbuka khadjia kawa chapombe
Changanyikiwa akawa mateka uuuhhh !
Baby wa dar es salama oooh ooh ! (dar es salaama ooh)

Sio wangu mimi bali wa dar es salaama
Kila binti mjini yeye amenpa mimba
Pita kila kona watoto humuita baba
Nilidhani wangu kumbe wa dar es salaama nzima

(Wa dar es salaama aaaah...)