DOWNLOAD SIDE CHICK BY LADY JAYDEE - MP3, MP4 & LYRICS

Side Chick Lyrics

Hukuwa hivyo, hukuwa hivyo
Wewe umebadilika
Hukuwa hivyo, hukuwa hivyo
Wewe umebadilika

Ulikuja ukiwa msafi mrembo
Shingo twageuza
Sifa zako zilienea huko mzima
Harufu wanukia kila kukicha

Mikogo yavutia kila ukipita
Hujipendi kama zamani kisingizio watoto
Kazi nazo hutaki fanua
Kisingizio watoto

Alivyokupenda jana
Ukabweteka ukanenepa
Alivyokukuta jana 
Si wa leo umebadilika

Usiwe hivyo, usiwe hivyo
Usimnyodoe mwenzio
Usiwe hivyo, usiwe hivyo
Usimnyodoe mwenzio

Usijioene umefika nawe waweza kupita
Haya mambo hayana mwenyewe side chick kumbuka
Oooh oooh waweza kupita
Aah aah aah hata wewe yatakwisha

Anavyokupenda leo 
Hata mwenzio alipendwa jana
Huduma zako leo
Huyo mwenzio alipewa jana

Huna muda wa kujiweka sawa
Hujipendi
Huna muda wa kujiweka sawa
Hujiwezi

Yote yanasemwa na wakilisha
Watu sio wema wana hakika
Ishi kwa makini ukijua lolote
Laweza tokea kwako au yeyote