DOWNLOAD MAGUFULI BAADAE BY LAVA LAVA - MP3, MP4 & LYRICS

Title Magufuli Baadae
Artists Lava Lava
Genres Bongo Flava
Country Tanzania

Magufuli Baadae Lyrics

Baadae, baadae
Magufuli baadae
Tutaonana baadae

Oooh baadae, baadae
Magufuli baadae
Tutaonana baadae

Oooh baadae, baadae
Magufuli baadae
Tutaonana baadae

Nenda salama baba
Si tupo bado twangojea
Japo tuna simanzi

Twakesha kwa ibada
Na dua njema tukuombea
Watoto kwa wazazi

Eeh ni mengi umetufanyia
Shukrani nahisi haitoshi
Kalale pema shujaa

Taifa lakulilia 
Twatamani urudi tufosi
Tumebaki na butwaa

Kusema ukweli ulituhusia
Tufanye na ibada
Wanafunzi kufeli hutaki sikia
Shule wasilipe ada

Za kisasa reli umetuachia
Ya juu madaraja
Viwanda vya ndege mambombadia
Mbona we hujavitumia baba?

Baadae, baadae
Magufuli baadae
Tutaonana baadae

Oooh baadae, baadae
Magufuli baadae
Tutaonana baadae

Natamani siku zirudi nyuma
Tukulipe japo theluthi ya wema wako
Ila haiwezekani, haiwezekani
Ila, ila, msalimie Nyerere baba

Baadae, baadae
Magufuli baadae
Tutaonana baadae

Oooh baadae, baadae
Magufuli baadae
Tutaonana baadae