DOWNLOAD AYA BY MARIOO - MP3, MP4 & LYRICS

Aya Lyrics

Mmmh,mmmmh 
Uwooo yeiye
(Mocco)
Mmmh,mmmmh

Ndo kusema kwamba nina bahati mbaya
Ama ni nyota imefifia ah
Maana sio kweli 
Kila siku mimi ndo  naumia

Ndo kusema kwamba sura yangu mbaya
Haina hulka ya kuvutia ah
Maana sio kweli 
Kila siku mimi ndo naumia

Ina maana penzi 
Lingekuwa chombo cha usafiri
Ningekosa hata sehemu ya kusimama
Ningewezaje? Nitawezaje?

Au labda mapenzi 
Hufaa kwa matajiri
Alafu mi hapa sina maana
Sa nitaanzaje? Nitaanzaaje?

Inawezekanaje nikose kufurahi 
Siku zote ninazoishi na uhai
Najua Mungu hapendi
Walimwengu mna visa

Nikisema niage nitakuwa najilaghai
Moyo utakuwa bado unanidai
Acha niweke imani
Ipo siku nitaridhishwa

Aya! Aya!
Aya! Aya!

Na sinacho maanisha mnakijua
Kuyakosa mapenzi inanitesa
Sawa nakua nayaona
Sa mbona yananizidia?

Hivi nacho maanisha mnakijua?
Upweke unanitesa
Halafu nakuwa nawaona
Wengine wanaenjoy(Aaah!)

Ingekuwa gambe  
Ndio dawa ya mawazo
Ningekunywa nilewe
Aah nilewe, nilewe

Inawezekanaje nikose kufurahi 
Siku zote ninazoishi na uhai
Najua Mungu hapendi
Walimwengu mna visa

Nikisema niage nitakuwa najilaghai
Moyo utakuwa bado unanidai
Acha niweke imani
Ipo siku nitaridhishwa

Aya! Aya!
Aya! Aya!

MoccoGenius!