DOWNLOAD INATOSHA BY MARIOO - MP3, MP4 & LYRICS

Inatosha Lyrics

Hata kama penzi maji masafi
Niacheni ninanawa
Maana yamenifika, yamenifika hapa

Ingawa nitakonda 
nimeridhia sawa
Maana kila dakika, mi huwa kilioni

Kukikucha macho juu 
Nakesha kulilia penzi
Kama kina nauguza mama eeh, mama eeh

Hapo shida sio heshima tu 
Hata wanamuingia wengi
Mwenzenu kupenda kashakata tamaa eeh, tamaa eeh

Oooh acha ikabaki ikawa historia, 
Japo sio kiroho safi
Ya nini kung'ang'ania biashara, tena yenye hasara

Na wala sisemi nitakuchukia, 
Japo moyo hautaki
Ya nini kung'ang'ana ng'ang'ana

Inatosha, inatosha
Inatosha, inatosha
Inatosha, inatosha

Ni kwamba moyo mashine 
Nina imani nitapoa
Hii hali siyo ya kudumu, nina imani nitapoa

Ni kwamba tumeumbwa kusahau 
Nina imani nitasahau
Hii hali siyo ya kudumu, nitakusahau

Kama kukupinga si ilishindikana
Sawa, sina chaguo
Maana japo, itanisumbua sumbua

Itani umbua umbua
Mchanga kwenye kitumbua, tumbua
Kwenye kitumbua, tumbua

Oooh acha ikabaki ikawa historia, 
Japo sio kiroho safi
Ya nini kung'ang'ania biashara, tena yenye hasara

Na wala sisemi nitakuchukia, 
Japo moyo hautaki
Ya nini kung'ang'ana ng'ang'ana

Inatosha, acha nipambane na hali yangu 
Inatosha, aaah mapenzi ya kupendwa, kushaka basi
Inatosha, mmmmh utaniniua
Inatosha, mmmh utaniua,mwenzako mie inatosha