DOWNLOAD SIMAMA BY MARISSA - MP3, MP4 & LYRICS

Simama Lyrics

Ama kweli dunia
Ni tambara mbovu lilotoboka
Moyo wangu vumilia 
Hifadhi makovu usijekuchoka

Wanatamani niwe bubu 
Kinywa changu nikose cha kusema
Nishangombana mpaka na ndugu
Chozi langu na bado sijakoma

Tena alazwe pema Ruge Mutahaba
Maneno yako najifunza leo 
"Penda unachopenda, usisumbuliwe na haya 
Mengine mengine kwa sababu usiwe driven away
Kwa kile unachopenda kwa vitu ambavyo
Haviongezi chochote kwenye kujenga passion 
Yako zaidi"

Mtaka moja kaitamani saba
Mtaani wanasema dhamana cheo eeh
Marissa simama, chenye mwanzo hakikosi mwisho
Marisa simama mama 
Marissa simama, chenye mwanzo hakikosi mwisho
Marisa simama ooh (Hakikosi mwisho)

Halaiti kama ardhi na mbingu vingeongea
Kuna mengi yalojificha 
Jua zama rafiki wa leo ndo adui wa kesho
Macho nafikicha

Oooh ni maisha ngombolela zinga
Nishabutua wakapata wengine
Kisa mwonekano kanipinga
Mara pap wanasema mengine

Tena alazwe pema Ruge Mutahaba
Maneno yako najifunza leo 
Mtaka moja kaitamani saba
Mtaani wanasema dhamana cheo eeh

Ninasimama
Mwanzo wa jiko sio mwisho
I don't  give up, I don't give up
Changamoto ndo maisha ya kila mtu atapitia
Don't give up