DOWNLOAD MUHUKUMU WA HAKI BY MARTHA MWAIPAJA - MP3, MP4 & LYRICS

Title Muhukumu wa Haki
Artists Martha Mwaipaja
Genres Gospel
Country Tanzania

Muhukumu wa Haki Lyrics

Parapanda itapigwa, itapigwa 
Parapanda itapigwa, itapigwa 
Parapanda itasika, itasikika 
Parapanda itasika, itasikika

Hapo ndipo mfalme wa haki atakapotawala 
Hapo ndipo mfalme wa kweli atakapotawala 
Maana dunia ya leo watu wanapendeleana
Maana dunia ya leo watu wanapendeleana

Atatawala mwenye dunia 
Atatawala mwenye watu wake
Maana dunia ya leo watu wanapendeleana 
Maana dunia ya leo watu wanapendeleana

Hapo ndipo falme zote za dunia zitanyamaza 
Mwenye wa kweli atawala 
Atasimamia mahakama zote kwa haki 
Atasimamia kesi zote kwa haki 
Kila mmoja atalipwa sawa

Dunia yote itatiishwa kwenye uweza wake 
Dunia yote itashangaa alivyo wa haki 
Mataifa watajua yeye ni mwema

Hapo ndipo wote tutajua kwamba yeye ni Baba 
Dunia yote itaelewa ni mhukumu wa haki 
Maana dunia ya leo watu wanasaidiana 
Maana dunia ya leo watu wanasaidiana

Atatawala asiyejua pendelea mwingine 
Watu wa leo wanatazama sifa ya mtu

Majira yanakuja ya kujua Baba wa kweli 
Majira yanafika watamjua Mungu wetu 
Leo hawatambua machozi tunayolia 
Leo hata ukilia hakuna wa kutazama

Hata ukiteswa hakuna wa kutazama 
Wakati unakuja Baba atatawala kwa haki 
Hapo ndipo falme zitajua yeye ni mfalme 
Hapo ndipo dunia itaelewa yeye ni Bwana

Tutapanguzwa machozi yetu na sisi 
Tutapanguzwa machozi yetu na sisi 
Tutaheshimiwa na dunia na sisi 
Tutaheshimiwa na watu wote na sisi

Hawawezi tambua haki yako leo hii 
Maana dunia ya leo watu wanasaidiana 
Hakuna wa kutetea maisha yako 
Maaana tawala za leo wanapendeleana

Anakuja mtawala wa haki kutusaidia 
Anakuja mtawala wa haki kutusaidia

Utafurahi na Baba 
Tutashangilia kwa Baba 
Maana falme wake Baba itakuwa ni yenye haki 
Maana falme wake Baba itakuwa ni yenye haki

Baba yetu atawala aah haa

Atatawala haaa (Atatawala Massiah Massiah)
Atatawala haaa (Atatuwala mwenye haki, Massiah)
Atatawala haaa (Atatawala, atatulipa wote)
Atatawala haaa  (Eeh baba, eeh baba)

Atatawala haaa (Atatubembeleza Baba)
Atatawala haaa (Atawala Baba, atatawala Baba)
Atatawala haaa (Atatawala, Massiah wetu)
Atatawala haaa (Atatulipa Yesu, Atatulipa Yesu)

Atatawala haaa (Eeh Baba, eeh Baba atatawala)
Atatawala haaa (Atawala, atatawala, atatawala)
Atatawala haaa (Atatawala kwa haki Baba atatawala)
Atatawala haaa (Ooooh, lalalala ha!)