DOWNLOAD BABA AKUPOKEE BY MWANAFA , OMMY DIMPOZ - MP3, MP4 & LYRICS

Baba Akupokee Lyrics

Umeacha pengo twamiss wako upendo
Ulikuwa nuru ukatutoa gizani
Uliyaishi matendo, mchapa kazi mzalendo
Daima twakushukuru mziba pengo ni nani?

Mi nawazaje sa itakuwaje
Watanzania wakuonapo macho umefumba
Mi nawazaje sa itakuwaje
Ooh Magu baba siamini ka umekwenda

Baba akupokee, baba akupokee
Baba akupokee, baba akupokee
Baba akupokee, baba akupokee
Baba akupokee, baba akupokee

Rais jiwe la katikati
Washwaligoma wakasanda
Ongea tupate dalili kwa sasa unataka kwenda
Tunakusahau vipi hata kama tukitaka
Barabara madarasa haki vyote vinatusuta

Chuma ni chuma kweli tena ni chuma cha pua
Mzigo mzito miaka sita dunia imekutambua
Nchi inazizima marafiki wanaona huruma
Vijana wako roho zimebaki zinauma

Hili ni deni zito
Mungu baba akupe pepo
Tuache na upako wako
Tuangalie huko uliko
Tunabaki watoto wako kwenye nchi yako
Nchi uloivaa na ukaipenda kwa moyo wako

Baba akupokee, baba akupokee
Baba akupokee, baba akupokee
Baba akupokee, baba akupokee
Baba akupokee, baba akupokee