DOWNLOAD USILIE BY NINI, WYSE - MP3, MP4 & LYRICS

Usilie Lyrics

Asubuhi imetimu, kumepambazuka
Kumekucha salama
Shida zinatulazimu haraka kuinuka
Kutafuta vya ngama

Namuona mama ameshika tama
Namuona baba amekata tamaa
Jirani yangu anaumwa sana
Kila kukicha afadhali ya jana

Usilie baba, usilie mama
Ah usilie dada futa machozi
Usilie kaka, usilie rafiki
Ah usilie ndugu futa machozi

Yametawala mawazo 
Na kila mara vikwazo
Ila changamoto ni funzo
Usikate tamaa

Taabu zinaturudia ila
Nguzo ni kuvumilia pia
Ushindi unakaribia tia
Dunia wee ee

Namuona dada ameshika tama
Namuona kaka amekata tamaa
Rafiki zangu wanashida sana
Kila kukicha afadhali ya jana

Usilie baba, usilie mama
Ah usilie dada futa machozi
Usilie kaka, usilie rafiki
Ah usilie ndugu futa machozi

Usilie, oooh aah
Na usikate tamaa

Tururutu....

Muda unakuja, na muda unafika
Usilie, don't don't cry
You don't cry, you don't cry
Inuka tena

(Free Nation)