DOWNLOAD SIO SIRI BY PRECIOUS ERNEST - MP3, MP4 & LYRICS

Sio Siri Lyrics

Sio siri tena, sio siri tena
Umenionyesha hio siri, ukanipa akili
Kupambana na hali zote
Sio siri tena, nasimama nakiri
We ni mwanga kwetu sote

Ulinionyesha njia nilipopotea
Ukanisamehe pale nilipokosea
Nitapaa sasa sauti nitasema milele
Utukufu usikike kote eeh

What I can see now
Ni uhuru na upendo naupata kwako ooh
Kwako oh oh oh oh

What I can feel now
Nasimama kwa kijasiri kwa uwezo wao
Wako oh oh oh oh

Itaniuma nisiposhukuru kwa kunipa upendo wote
Afya na nguvu zote sio siri tena aah
Malaika wa Bwana mimi anilinde siku zote
Mchana usiku kote sio siri tena aah

Bubu haongei, kipofu haoni
Kiziwi hasikiii ni imani tu
Wagonjwa vitandani, watoto mitaani
Mlinzi wao ni nani? Ni wewe tu

Tunakuomba Baba, weka mikono yako
Shusha uponyaji kwetu, sio siri tena aah
Tunaziomba Baba hizo baraka zako
Bariki nyumba zetu, sio siri tena

Itaniuma nisiposhukuru kwa kunipa upendo wote
Afya na nguvu zote sio siri tena aah
Malaika wa Bwana mimi anilinde siku zote
Mchana usiku kote sio siri tena aah

Kwa imani jina lako nalisema
Kama ni roho yangu itapona
Hakuna siri tena mi naona
Sio siri tena