DOWNLOAD PAMBANA BY SAI KENYA - MP3, MP4 & LYRICS

Pambana Lyrics

SHIRKO

Muda mwingine ukikaa unawaza
Kwanini mambo hayaendi sana
Labda pengine watu wanakukwaza
Hawakupendi wanakuona chawa

Ukiendelea kidogo tu tatizo
Wanataka uishi maisha maigizo
Ikosifuraha iende likizo
Usikate tamaa

Ndio maana nataka ujitume
Gurudumu lisukume
Maisha ni changamoto
Na si rahisi kutimiza ndoto

Ndio maana nataka ujitume
Gurudumu lisukume
Ili uwake moto 
Lazima kuni ziungue

Pambana! We kaka pambana pambana
Pambana! We dada pambana pambana
Pambana! Na hali yako 
Mwisho utafanikiwa

Pambana! We baba pambana pambana
Pambana! We mama pambana pambana
Pambana! Na hali yako 
Mwisho utafanikiwa

Ukianza biashara yako ndogo
Watakuiga wakishindwa wataiponda
Na ukinyamaza watakuona mdogo
Watakupinga watavunja moyo utakonda
Sio pekee yako

Kenyatta naye alipambana
Cheki sasa tulipo
Mekatilili naye aling'ang'ana
Ona sasa tulipo

Sasa wewe
We ni nani usipambane
Ufike uendako, uendako maaana

Usilewe sifa jikusanye
Kisha deki maisha yako
Oooh yako jitahidi ng'ang'ana

Ndio maana nataka ujitume
Gurudumu lisukume
Maisha ni changamoto
Na si rahisi kutimiza ndoto

Ndio maana nataka ujitume
Gurudumu lisukume
Ili uwake moto 
Lazima kuni ziungue

Pambana! We kaka pambana pambana
Pambana! We dada pambana pambana
Pambana! Na hali yako 
Mwisho utafanikiwa

Pambana! We baba pambana pambana
Pambana! We mama pambana pambana
Pambana! Na hali yako 
Mwisho utafanikiwa