DOWNLOAD NI SALAMA ROHONI (TENZI ZA ROHONI) BY SHEDDY - MP3, MP4 & LYRICS

Title Ni Salama Rohoni (Tenzi za rohoni)
Artists Sheddy
Genres Gospel
Country Tanzania

Ni Salama Rohoni (Tenzi za rohoni) Lyrics

Nionapo amani kama shwari
Au nionapo shida
Kwa hali zote umenijulisha
Ni salama rohoni mwangu

Salama Salama
Rohoni Rohoni
Ni salama rohoni mwangu
Nionapo amani kama shwari

Ingawa Shetani atanitesa
Nitajipa moyo kwani
Kristo ameona unyonge wangu
Amekufa kwa roho yangu

Salama Salama
Rohoni Rohoni
Ni salama rohoni mwangu

Dhambi zangu zote wala si nusu
Zimewekwa Msalabani
Wala sichukui laana yake
Ni salama rohoni mwangu

Salama Salama
Rohoni Rohoni
Ni salama rohoni mwangu

Ee Bwana himiza siku ya kuja
Panda itakapolia
Utakaposhuka sitaogopa
Ni salama rohoni mwangu

Salama Salama
Rohoni Rohoni
Ni salama rohoni mwangu