DOWNLOAD ANGERUDI BY TOMMY FLAVOUR - MP3, MP4 & LYRICS

Angerudi Lyrics

Ooh moyo machungu nitashindwa nisiumie
Machozi yatazidi nisijizuie
Bora ingekuwa ndoto inipitie
Siwezi amini we haupo nami

Sio ndoto sina nguvu hata vipi nihadithie
Watalibeba aje ndugu zangu mie
Majonzi huzuni utuwachie
Baba pumzika kwa amani

Ooh Mungu nakuomba Baba uliye juu nusuru
Naona mzito mtaani huu utakwendaje?
Nishapoteza kiongozi mkuu 
Mbele giza totoro 
Kama ningeweza ningekwomba Mola

Angerudi angerudi angerudi
Angerudi hamna kama yeye (Mola ningekuomba)
Angerudi angerudi angerudi
Angerudi hamna kama yeye

Hata sekunde
Hata dakika hata dakika tu
Ooh baba

Kwenye shida na matatizo ulitutetea wewe
Kimbilio la malalamiko ulitubeba wewe
Nuru imezima umetuacha wenyewe
Vingi umetuachia jicho lako la mwewe

Nakuomba Baba uliye juu nusuru
Naona mzito mtaani huu utakwendaje?
Nishapoteza kiongozi mkuu 
Mbele giza totoro 
Kama ningeweza ningekwomba Mola

Angerudi angerudi angerudi
Angerudi hamna kama yeye (Mola ningekuomba)
Angerudi angerudi angerudi
Angerudi hamna kama yeye

Angerudi angerudi angerudi
Angerudi hamna kama yeye (Oooh Mola wangu)
Angerudi angerudi angerudi
Angerudi hamna kama yeye