DOWNLOAD MUNGU WA NYAKATI ZOTE ( GOD OF ALL TIMES) BY UPENDO WISDOM K - MP3, MP4 & LYRICS

Title Mungu wa Nyakati zote ( God of all Times)
Artists Upendo Wisdom K
Genres Gospel
Country Tanzania

Mungu wa Nyakati zote ( God of all Times) Lyrics

Mungu wa nyakati zote, nakuabudu
Mungu wa wote wenye mwili, nakuabudu
Mwenye mamlaka yote, nakuabudu
Wewe ni Mungu wa nyakati zote

Mungu unayeishi, nakuabudu
Mungu unayejibu, nakuabudu
Mzee wa siku, nakuabudu
Wewe ni Mungu wa nyakati zote

Milimani mabondeni, gizani nuruni
Kiangazi au masika Kwenye raha au majonzi
Mkono wako waokoa, roho wako wafariji
We ni Mungu wa nyakati zote

Haulinganishwi na chochote
Hautetemeshwi na majira
Ulikuwako sasa uko na milele
Na milele utadumu

Alpha Omega mwanzo mwisho
Watangaza mwisho kabla ya mwanzo
Wewe ni Mungu wa nyakati zote

Ee Mungu mwenyezi, nakuabudu
Mungu mwenye enzi, nakuabudu
Mshika maagano, nakuabudu
Uweza wako ni wa ajabu

Mungu mtukufu, nakuabudu
Mungu mtakatifu, nakuabudu
Mungu mkamilifu, nakuabudu
Uweza wako ni wa ajabu

Wastahili Bwana, wastahili Bwana
Wastahili Bwana, wastahili Bwana
Wastahili Bwana, wastahili Bwana
Wewe ni Mungu wa nyakati zote

Unaweza Bwana, unaweza Bwana
Unaweza Bwana, unaweza Bwana
Unaweza Bwana, unaweza Bwana
Uweza wako ni wa ajabu

Yesu uweza wako ni wa ajabu
Wewe ni Mungu wa nyakati zote