DOWNLOAD USINIJARIBU BY WINI - MP3, MP4 & LYRICS

Title Usinijaribu
Artists Wini
Genres Bongo Flava
Country Tanzania

Usinijaribu Lyrics

Chozi la furaha
Mpaka nashangaa
Linanitokaa

Mmmh, ndugu ndugu kifuani
Lilonisumbua mimi
Linanitoka

Kwani hisia ziliniumiza
Kwenye moyo wangu 
Nabaki nalia, nalia oooh aah

Mchana niliona kiza
Eeh Mola wangu
Mapenzi balaa, ooh ah...

Nilipiga magoti 
Nikaota sugu kwenye miguu
Kubembeleza mapenzi

Nikamhonga honga
Nikatoa pesa kwenye vibubu
Ninakopenda sipendwi

Nishaumwa na nyoka 
Mwenzako naogopa majani
Nisije nikakupa moyo wangu 
Ukaeka rehani

Usinijaribu(Ooh wee eeh)
Danganya toto sitaki
Usinijari-ii, usinijaribu

Usinijaribu(Ooh wee eeh)
Danganya toto sitaki
Usinijari-ii, usinijaribu

Usini petipeti
Nikazama mazima 
Nikashindwa kutoka
Mwisho ukaniacha nalia

Usinidanganye
Usinichanganye
Unifanye kilema wa mapenzi
Magongo uyashike weee

Nijibane bane(aiya)
Furaha upate wee(aiya)
Unifanye ka fisi mifupa
Minyama unakula wee

Nilipiga magoti 
Nikaota sugu kwenye miguu
Kubembeleza mapenzi

Nikamhonga honga
Nikatoa pesa kwenye vibubu
Ninakopenda sipendwi

Nishaumwa na nyoka 
Mwenzako naogopa majani
Nisije nikakupa moyo wangu 
Ukaeka rehani

Usinijaribu(Ooh wee eeh)
Danganya toto sitaki
Usinijari-ii, usinijaribu

Usinijaribu(Ooh wee eeh)
Danganya toto sitaki
Usinijari-ii, usinijaribu